Wednesday, August 09, 2006

Darwin's Nightmare & JK: The Response

Fellas,

This is not my original thought, but it came from one of my closest buddies. I will post it in its entirety. Very interesting perspective from my point of view, but you be the judge.

+++++
Rais wa Tanzania ni mtu mkubwa sana. Na tena anawakilisha 'the whole institution of the presidency'. Kwa yeye kujiingiza kwenye malumbano na mtu binafsi tu, tena raia wa nchi nyingine, haileti picha nzuri. Kuna namna nyingi za kuweza kupinga yale yaliyosemwa na kuonyeshwa kwenye filamu hiyo ya Darwin's Nightmare. Rais Kikwete amefanya 'tactical errors' kubwa mbili hapa.

Ya kwanza inahusu hiyo 'confrontation' na mtengenezaji wa filamu huko Paris, France wakati wa ziara yake huko na kudai kuwa apewe 'evidence' kuhusu madai hayo yaliyoko kwenye filamu. Yaani rais mzima wa nchi anakosa kazi na kuanza kuwafuatilia private citizens wa nchi nyingine? Kulikuwa na umuhimu gani wa rais kukutana na huyu jamaa huko Paris? Isitoshe, filamu za mtindo wa 'documentary' kwa kiasi kikubwa ni maoni binafsi ya mtengenezaji. Kwa hiyo mtengenezaji atavutia zaidi kwake na kupiga picha zile zinazounga mkono mtizamo wake. Kwa mfano kwa walioko Marekani mtakumbuka kuwa kuna jamaa mmoja alitengeneza filamu ya Farenheit 9/11. Filamu hii ilikuwa inamwandama Rais George W Bush. Lakini hata siku moja sikumsikia Rais Bush akilumbana na bwana Moore kuhusu hiyo filamu.

Ya pili inahusu hoja alizotoa mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa mkutano wake na wazee wa mkoa wa Mwanza. Hata kama tukichukulia kuwa alikuwa anaongea na 'a partisan crowd', na kuwa chochote atakachosema basi kitashangiliwa kwa nderemo na vigelegele. Kuna msemo kuwa maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga, kwa maantiki hayo rais wetu angepaswa kujibu mapigo yote ya kwenye filamu hiyo hoja kwa hoja na sio vinginevyo. Ni kweli kuwa kuna ukahaba wa hali ya juu huko Ufaransa, na kuwa watu wanakata leseni ya kuwa makahaba. Lakini 'that was not the central issue' kwenye filamu hiyo, na wote tunajua hivyo. Juhudi zozote za kufanya 'deflection' kutoka kwenye ujumbe wa filamu hiyo 'is not a good rebuttal strategy'.

Nilipata bahati ya kusikia interview ya huyu Hubert Sauper kwenye National Public Radio (NPR). Bonyeza tovuti hii hapa chini ili uweze kusikia hayo mahojiano. Kwa maneno yake mwenyewe bwana Hubert anaongelea sababu zilizomfanya atengeneze hiyo filamu.
http://www.npr.org/templates/story/story.php?storyId=5227735

Kwa hiyo hili sio suala la kuwa wazungu fulani wanataka kuendelea kutunyanyasa sisi waafrika kwa kutengeneza filamu mbaya kuhusu maisha yetu. Sidhani kama maoni mengine kwenye suala hili zima yamekita kwenye uchambuzi yakinifu wa filamu hii.

Source: Seppy.
+++

1 comment:

Jeff Msangi said...

Kwa bahati nzuri au mbaya mimi binafsi nimeshakuwa na mazungumzo ya kina na mtengeneza filamu huyu anayezungumziwa. Niliwasiliana naye juu ya mambo ambayo binafsi niliyaona yalikuwa innacurate.Tatizo langu la kwanza lilikuwa ni tafsiri mbovu ya kutoka kiswahili kwenda kiingereza.Kama umeitazama hiyo documentary utagundua kwamba walichokuwa wakikisema waliohojiwa sicho kilichotafsiriwa.Badala yake mtengeneza filamu huyu alikuwa anawatilia kinywani maneno aliowahoji.Labda hii ndio hiyo bias mshikaji wako anayoionglea.

Kwa mtizamo wangu nadhani raisi hakuwa na malumbano ya moja kwa moja na Sauper bali kuwaambia wananchi "siasa". Kuna ukweli mwingi tu katika documentary ile ila ushahidi wa wazi ndio ambao nadhani Kikwete alikuwa anaupinga.Huko Ufaransa sio kwamba Kikwete alimfuata huyu jamaa ila jamaa alijipenyeza mpaka akaonana na Kikwete uso kwa uso.Kikwete alifanya vizuri kumuuliza kuhusu ushahidi wake.Filamu ya Michael Moore ya Farehheit 9/11 ilikuwa gumzo kubwa la nyumba nyeupe kama mtakumbuka.Ilikuwa mbinde kuitoa ile filamu.Bush aliiongelea sana tu.Ushahidi upo mtandaoni.

Mkumbuke kwamba filamu ile imeianika Tanzania dunia nzima.Ilikuwa nominated kwa ajili ya Oscar.Kikwete asipojaribu kuonyesha upande mwingine wa shilingi nani afanye hivyo? Yeye kama raisi ana wajibu wa kuitetea nchi yake hata kama habari husika ina utata.Nadhani hajakosea kuliongelea hilo na wazee wa Mwanza ingawa nadhani kulikuwa na haja ya yeye kujua undani zaidi wa alichokuwa anakiongelea kwa minajili ya "kukanusha"